Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Michael Travis Leake, mwanamuziki wa Marekani, azuiliwa Urusi

Michael Travis Leake, Mwanamuziki Wa Marekani, Azuiliwa Urusi Michael Travis Leake, mwanamuziki wa Marekani, azuiliwa Urusi

Mon, 12 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Mahakama ya Urusi imemzuilia raia wa Marekani Michael Travis Leake, mwanamuziki na mwanajeshi wa zamani wa paratrooper, kwa tuhuma za kutumia dawa za kulevya.

Mahakama ya Khamovnichesky ya Moscow ilidai kuwa Bw Leake "alipanga uuzaji wa dawa za kulevya kwa vijana", AFP iliripoti.

Hata hivyo, anakanusha mashtaka hayo.

Televisheni ya serikali ya Urusi ilitangaza kanda ya kesi ya Bw Leake iliyomuonyesha akiwa amefungwa kwenye ngome ya chuma.

Katika video tofauti iliyoshirikishwa mtandaoni, alisema "hakujua" kwa nini alizuiliwa.

Huku akionekana kuchanganyikiwa, alisema haamini kuwa amefanya kile anachotuhumiwa, kwa sababu hajui ni mashtaka gani.

The department was closely monitoring the case, the spokesperson added.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alisema wafanyakazi wa ubalozi walihudhuria kusikilizwa kwa kesi ya Bw Leake siku ya Jumamosi, 10 Juni.

Idara ilikuwa ikifuatilia kesi hiyo kwa karibu, msemaji huyo aliongeza.

Atazuiliwa rumande hadi tarehe 6 Agosti, AFP iliripoti.

Bw Leake ni angalau Mmarekani wa tatu kuzuiliwa nchini Urusi katika miaka ya hivi karibuni huku kukiwa na mvutano mkali kati ya Washington na Moscow.

Mwanamuziki na mtayarishaji wa muziki aliripotiwa kuishi nchini Urusi kwa miaka mingi, Bw Leake alikuwa mwanachama wa Lovi Noch, "bendi ya muziki ya Marekani" iliyoko Moscow.

Chombo cha habari cha Marekani CNN kiliripoti kwamba alionekana kwenye kipindi cha usafiri cha Parts Unknown - kilichoandaliwa na mpishi marehemu Anthony Bourdain - kwa kipindi cha 2014 ambacho kilirekodiwa huko Moscow na St Petersburg.

Darya Tarasova, ambaye alitayarisha kipindi hicho, aliiambia CNN kwamba Bw Leake alikuwa "mtangazaji" ambaye "alizungumza sana" na "aliyependa Urusi".

Mara nyingi alifanya kazi na bendi za hapa, Bi Tarasova alisema.

Vyombo vya habari vya Urusi viliripoti mapema kukamatwa kwake katika nyumba yake huko Moscow.

Maafisa wa Marekani hapo awali waliishutumu Urusi kwa kuwalenga kimakusudi raia wa Marekani ili kuwakamata.

Mnamo Machi, mamlaka ya Urusi ilimkamata mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich, mwandishi wa Wall Street Journal, kwa mashtaka ya ujasusi.

Bado anaendelea kuzuiliwa kabla ya kesi inayomkabili kusikilizwa.

Mwishoni mwa mwaka jana, mchezaji wa mpira wa vikapu wa Marekani Brittney Griner, ambaye alifungwa nchini Urusi kwa mashtaka ya madawa ya kulevya, aliachiliwa kwa kubadilishana wafungwa kwa muuzaji silaha wa Kirusi Viktor Bout

Mwanajeshi wa Marekani Paul Whelan anatumikia kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya "kijasusi" - alihukumiwa kabla ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, ambako kumedhoofisha uhusiano kati ya Marekani na Urusi.

Chanzo: Bbc