Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Miaka 70, siku 274 za Utawala wa Malkia Elizabeth II

Malkia Malkia Elizabeth wa Uingereza enzi za uhai wake

Sat, 10 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Malkia Elizabeth II anakuwa kiongozi pekee aliyetawala kwa muda mrefu zaidi katika historia ya kifalme balani Ulaya, huku akiwa mtawala wa Uingereza aliyetawala kwa muda mrefu zaidi ikiwa ni jumla ya miaka 70 na siku 274.

Taarifa za kifo cha Malkia Elizabeth II kilichotokea katika jumba la kifalme Septemba 8 huko Uskoti na kuchapishwa katika ukurasa rasmi wa Tweeter wa familia ya kifalme mapema Septemba 8, 2022.

Mwaka 1926 Elizabeth Alexandra Mary Windsor alizaliwa Mjini London Uingereza na mwaka 1947 Novemba 21 alifunga ndoa na Philip Mountbatten. Februari 6, 1952 Elizabeth akawa Malkia wa Uingereza kufuatia kifo cha baba yake Mfalme George VI aliyefariki kwa maradhi ya saratani. Na Juni 2, 1953 alitawazwa rasmi kuwa malkia wa Uingereza huko Abbey Westminster.

Hata hivyo, tarehe 9 Aprili, 2021 mume wa Malkia Elizabeth, mwanamfalme Philip alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 99. Na baadaye mwaka huu 2022 Malkia Elizabeth II amefariki akiwa na miaka 96.

Wakati wa utawala wake Malkia Elizabeth II aliwashuhudia mawaziri wakuu 15 ingawa Ali jitahidi sana kutoonesha upande wake kisiasa lakini alikuwa akikutana na viongozi wa kisiasa Mara kwa mara. 

Malkia Elizabeth II alikuwa kiongozi Mkuu wa mataifa 16 huku akiwa kiongozi mkuu wa Kanisa la Anglikana. Wakati akiwa Malkia ametembelea mataifa zaidi ya 110 kote ulimwenguni.

Sasa, baada ya miaka 70 kupita Uingereza imempata kiongozi mwaume ambapo kwa mujibu wa taratibu za kifalme ni kwamba mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth II ambaye ni Prince Charles mwenye miaka 73 atakuwa Mfalme na mtawala mkuu wa Uingereza, ataitwa Mfalme Charles III.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live