Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miaka 27 ya kifo cha 2Pac, nadharia ya kifo chake inatisha

2pac18 2Pac Shakur.

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imetimia miaka 27 siku ya leo tangu kifo cha rapa maarufu duniani, 2Pac Shakur aliyefariki Septemba 13, 1996 baada ya kulazwa hospitali kwa siku 6 kuokoa maisha yake ambapo alipigwa risasi akiwa ndani ya gari Septemba 07, 1996, mjini Las Vegas Marekani.

Jina lake la kuzaliwa ni Tupac Amaru Shakur, lakini wengi wanamfahamu kwa jina la 2Pac au Makaveli, alizaliwa June 16,1971.

Tupac alifariki akiwa na umri wa miaka 25, aliacha album 5 na pia anatajwa katika orodha ya wasanii bora wa hiphop wa muda wote.

Enzi za uhai wake aliwahi kuingia kwenye Guinness World Record kutokana na mauzo ya album yake kutajwa kufikia milioni 74 Dunia nzima lakini milioni 44 kwa mauzo ya Marekani pekee kama msanii wa muziki wa Hip Hop.

Marehemu 2Pac alitamba na ngoma nyingi kali zikiwemo Hit Em Up, Dear Mama, Only God Can Judge Me, Life Goes On na nyingine nyingi aliwahi pia kushiriki kwenye filamu mbalimbali ikiwemo Poetic Justice akiwa na Janet Jackson , Above the Rim, Juice.

Moja ya Interview za Tupac za kukumbukwa ni hii alivyosema. “Everybody rap, we don’t rap, we rap to make money, we do busness… Msanii wa Bongo Fleva chukua hiyo.

Tangu wakati huo, kumekuwa na mijadala huku baadhi ya mashabiki na watu wa karibu wakiamini kwamba 2pac, hakufa yupo hai, huku baadhi ya mashabiki na watu wakaribu Wanaamini 2Pac alifariki.

Wanaamini 2Pac yupo hai kutokana na sababu Fulani ambazo Zina uthibitisho ndani yake. Kuna video ilitolewaga na suge knight, rafiki wa 2pac, ikimwonesha yupo na 2pac na kusema 2Pac yupo Cuba.

Pia mwaka 2018 mtoto wa Suge Knight alionyesha video ya 2Pac na kusema yupo Malaysia.

Wengine wanaamini 2Pac alifake kifo chake ndiyo alitumia jina la Machiaveli, ambapo mwenye jina hilo alikuwa Nicole Machiaveli, ambaye nae alisha fake kifo chake na ukilichanganua jina hilo Lina maana " Am a live".

Lakini kuna nadharia ambayo inasema kuwa 2pac alikufa kweli, na walitaka kumclone /copy lakini ilishindikana kwasababu Kifo chake kilikuwa hadharani.

Kwa sababu hiyo, walitengeneza propaganda zaku aminisha watu kuwa yupo hai, kwa kutengeneza video na picha, na kuwatumia watu wa karibu na 2Pac kusambaza video hizo, ili iwe rahisi kwa watu kuamini na kuwa attention na jambo hilo.

Hivyo ikitokea siku wakafanikisha lengo lao la kumludisha watu wasiwe na hoja kwasababu tayari walisha aminishwa .

Na hii plan inasemekana ilitengenezwa kutoka kipindi anakufa ndiko sababu hata mwili wa 2Pac haukuzikwa, ulichomwa moto na majivu yalimwagwa kwenye bustan ya stone mountain Georgia, kwenye sanamu yake huku mengine yali vutwa kama sigara na jamaa zake wa kundi la Ki-Illuminat.

Ili kufuta uthibitisho ndio sababu mpaka leo hii hakuna kaburi la 2Pac, ili kusudi watakapo mtengeneza mpya kusiwe na ushahidi wowote wa kifo chake.

Je ulianza kuwa shabiki wa Tupac kupitia wimbo gani?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live