Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhe. Shonza aibuka baada ya matusi ya Diamond

5084 Db03cf7ebc 3 TZW

Tue, 20 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amedai kuwa hawezi kumjibu Diamond Platnumz kwa kuwa hajafuata utaratibu wa serikali.

Naibu Waziri Juliana Shonza (katikati)

Akiongea na Mwananchi Digital, Mhe. Shonza, amesema, “Serikali huwa haijibu vitu ambavyo vimezungumzwa kwenye social media, tunautaratibu wetu. Mtu kama ana malalamiko alete ofisini au aandike barua ndio utaratibu wa kazi.”

“Kwa hiyo Damond siwezi kumjibu nampuuza kwa sababu kwanza hajafuata utaratibu,” amesema Naibu Waziri. Serikali haiwezi kupoteza muda kubishana na mtu mmoja, mimi siwezi kujibia vitu ambavyo mtu ameongea kwenye radio, mimi najibu vitu ambavyo mtu ameleta ofisini,” ameongeza.

                                  Diamond akiwa studio za Times FM

Diamond jana (Jumatatu) kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM, alimjia juu Naibu Waziri Shonza kwa madai ya kuzifungia nyimbo za wasanii wakati kama wasanii wanaenda kinyume ni jambo la kuelekezana.

“Suala si kufungia tu nyimbo, mimi ukinifungia nyimbo hainipunguzii kitu nikienda nje naenda nai-perform ukiwa hutaki sinaondoka tu naenda nchi nyingine, kwa hiyo ni kukaa tuzungumze, tuelekezane lakini tusifanye kama kukomoana, hapana, tufanye katika mazingira ambayo yatasaidia sanaa ikue,” alisema Diamond.

“Bongo Flava naijua kweli kweli, halafu kama mimi ni mtu ambaye siogopi kwenda jela kwa ajili ya Bongo Flava, siogopi kufanya chochote kwa sababu ndio Baba yangu na Mama yangu ndio nimefanya hadi nimefika hapa, kwa hiyo unapo-deal na sanaa yangu hakikisha unafanya kitu ambacho kipo sahihi usikurupuke kwa sababu una mamlaka,” amesisitiza.

Chanzo: bongo5.com