Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mhalifu atangaza dau nono la pesa ili Gavana wa Serikali akamatwe

Portrait Of Pirate Jean Lafitte Jean Lafitte

Sun, 7 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Je Wajua? Anaitwa Jean Lafitte, alizaliwa mjini Bordeaux Ufaransa mwaka 1780.

Huyu mwamba alikuwa Haramia, na mvamizi mkubwa wa meli za wafanyabiashara baharini aliyeogopeka sana kwenye karne ya 18.

Uhalifu wake mwingi alikuwa akiufanyia Amerika, Ulaya na katika nchi za Mexico pamoja na Uhispania.

Kwa jeuri aliyokuwa nayo aliweza kumiliki zaidi ya wafanyakazi 200 wa kike pamoja na wa kiume.

Kutokana na Lafitte kuonekana kero na tishio, gavana mmoja wa serikali ya Hispania aliwahi kutangaza dau kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa wa haramia huyo basi angezawadiwa $500 (milioni moja na laki 3 ya kitanzania).

Cha kufurahisha sasa, Jean Lafitte naye akatangaza dau kwa yeyote atakayefanikisha ukamatwaji wa Gavana huyo basi atamzawadia $5,000 (takriban milioni 12.9 za kibongo. Ikabidi mpango wa Gavana ufe jamaa akaendelea mishe zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live