Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mfanyakazi feki wa Benki akimbiwa na mke baada ya kugundulika ni "Tax Driver"

25341e729725b053 Mfanyakazi feki wa Benki akimbiwa na mke baada ya kugundulika ni "Tax Driver"

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Jackline Wanjiru amemkimbia mumewe baada ya kugundua kuwa bwana harusi Alfred Musa alimdanganya kuwa ni mfanyakazi wa benki kumbe ni dereva wa teksi.

Wawili hao wamechumbiana kwa kipindi cha miaka minne.

Tukio hilo limetokea siku ya Jumatano, Septemba 22, baada ya hafla ya harusi kufutwa katika kaunti ya Kilifi kutokana na bibi harusi kutoroka kanisani.

Juhudi za marafiki zake bwana harusi kujaribu kumrejesha kanisani ili sherehe hiyo iendelee ziligonga mwambaKweli kuishi kwingi ndio kuona mengi na njia ya mwongo kawaida ni fupi.

Jackline Wanjiru alikimbia kutoka Kanisa la AIC Mbeeni, muda mfupi kabla ya harusi yake baada ya kugundua kuwa bwana harusi Alfred Musa alimdanganya kuwa ni mfanyakazi wa benki kumbe ni dereva wa teksi.

Katika kipindi cha miaka minne ya mahusiano yao, Alfred alikuwa amemwambia Jackline kuwa yeye ni mfanyakazi wa Benki ya KCB katika tawi la Malindi.

Hata hivyo, Wanjiru alipogundua kuwa mumewe anafanya kazi kama dereva wa teksi, aliamua kukimbia katikati ya shughuli ya harusi yake na kuwaacha wageni kwa mataa.

Bwana harusi avunjwa mgongo na marafiki siku yake ya harusiKatika tukio lingine katika harusi, Tuko.co.ke iliripotia kuwa bwana harusi aligeuka kuwa mgonjwa katika hafla yake ya harusi baada ya kuangukia kichwa chake.

Kisa hicho kilitokea katika harusi moja kaunti ya Bihor, Kaskazini Magharibi mwa Romania wiki moja iliyopita.

Kwa mujibu wa The Sun, bwana harusi huyo aliporushwa hewani mara ya kwanza, alidakwa lakini katika jaribio la pili aliangukia kichwa na kumsababishia jeraha mbaya.

Daktari wa hospitali ambapo bwana harusi huyo alipelekwa kwa matibabu alizungumzia hali yake akisema aliumia uti wake wa mgongo na anahitaji kufanyiwa upasuaji.

Bwana huyo mwenye umri wa miaka 31, amesema amemfahamisha wakili wake akitaka kuwashtaki marafiki zake kwa kumsababishia jeraha.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke