Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mfalme mtarajiwa Jordan kufunga ndoa

Rajwa Alseif.jpeg Mfalme mtarajiwa Jordan kufunga ndoa

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jordan inajiandaa kwa harusi ya Kifalme itakayofungwa Alhamisi hii ambapo Mwana Mfalme Hussein (28) ambaye ni Mfalme mtarajiwa, atafunga ndoa na Rajwa Alseif (29).

Ndoa hiyo itafungwa katika Kasri ya Zahran mahali ambapo baba yake na Hussein, Mfalme Abdullah II na babu yake marehemu Mfalme Hussein walifungia ndoa zao.

Mke wa Rais wa Marekani, Jill Biden anatarajia kuwepo kwenye shughuli hiyo itakayohudhuriwa na wanafamilia za kifalme kutoka pande mbalimbali za dunia.

Sherehe za ndoa hiyo zilianza rasmi wiki iliyopita kwa sherehe ya Henna iliyoandaliwa na mama wa bwana harusi Malkia Rania wa Jordan na kuhudhuriwa na mamia ya wanawake.

Bibi harusi anatokea Saudi Arabia,ana shahada ya usanifu ( Architecture) kutoka Chuo Kikuu cha Syracuse ,New York, pia ameishi na kufanya kazi jijini Los Angeles.

Baba wa bibi harusi ni mwanzilishi wa Makampuni makubwa ya uhandisi ya nchini Saudi Arabia na mama yake ni ndugu yake Mfalme Salman wa Saudi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live