Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu mwanamke mwenye Nywele nyingi zaidi duniani

Nywele Kibao Mfahamu mwanamke mwenye Nywele nyingi zaidi duniani

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supatra 'Natty' Sasuphan kutoka nchini Thailand anashikilia rekodi ya dunia(Guiness World Records) kwa kuwa msichana mwenye nywele zaidi mwilini tatizo ambalo kutoka zama za kati hadi sasa watu 50 ndio rekodi zao zipo kwakuwa na hali hiyo

Supatra alizaliwa Agosti 5, 1999 akiwa na nywele, mama yake alitaka kukimbia hospitali kwa mshituko, madaktari hawakumpa ruhusa ya kuondoka kwa kuona atamuacha mwanae, hata hivyo baba mtu alisema huyo ni mtoto wao lazima wamlee kwa mapenzi yote na wana bahati amezaliwa katika familia yao.

Mama na baba yake wamemlea kwa mapenzi yote kiasi cha Supatra mwenyewe kuwashukuru wazazi wake kwa kutomtenga wala kumlea katika mazingira ajione tofauti na wengine. Supatra amesema wazazi wake walimlea kwa kujivunia kuwa nae na walikuwa nae popote walipoenda.

Mwaka 2018 Supatra alipata mchumba alienae(picha katika comments) na kuolewa ambapo walianza kuwa kama marafiki na baadaye wakaanza kupendana. Baada ya kuolewa huwa anazinyoa nywele zake ambazo baada ya muda zinakua tena kwasababu tatizo lake halina tiba ya kudumu hadi sasa.

Supatra amesema hajioni kuwa tofauti na wengine isipokuwa anajiona special kwa kuwa na nywele nyingi.

Amesema haikuwa rahisi maisha aliyopitia sababu sehemu ya jamii, ikiwemo shuleni alikuwa akidhihakiwa na wenzie kwa kuitwa majina ya kuudhi lakini tangu mwanzo aliamua kutoishi maisha ya upweke, pia aliamua kuishi kwa kutowapa nafasi watu wenye mitazamo hasi ili wasizidi kumuathiri[kisaikolojia]

Amesema aliamua udhaifu au changamoto yake aigeuze kuwa nguvu kwake aishi vizuri. Tangu mwanzo Supatra alikuwa na malengo ya kuwa mfanyakazi wa serikali ili kuisaidia jamii, jamii ambayo ilikuwa ikimdhihaki kwa hali aliyonayo.

Amesema kulelewa na wazazi wake kwa upendo wote, baadaye kuwa na mpenzi, kupendwa na kuolewa ni moja ya vitu vilivyompa furaha na kusonga mbele na maisha.

Mwaka 2010 ndio aliweka rekodi ya dunia (Guiness World Records) kwa kuwa msichana mwenye nywele nyingi mwili, nywele hizo zipo sehemu kubwa ya mwili wake isipokuwa katika viganja vya mikono, nyayo za miguu nakadharika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live