Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu mtoto Mtanzania anayeigiza Netflix

Mtoto Asha.png Mfahamu mtoto Mtanzania anayeigiza Netflix

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto mwenye asili ya Tanzania, Ridley Asha Bateman ambaye anaishi nchini Canada na wazazi wake Loyd Bateman na Rachel Luttrell ni mwigizaji Mdogo aliyezaliwa mwaka wa 2012 na kupata bahati ya kuingia Netflix kupitia filamu ya LOU.

Katika mahojiano aliyofanyiwa na moja ya vyombo vya habari, Asha amesema kwamba mama yake na bibi yake wamezaliwa Tanzania na wamekuwa wakimfundisha Kiswahili tangu akiwa mtoto.

Kupitia ukurasa wa mtangazaji maarufu nchini Tanzania, Fredrick Bundala alimaarufu @skytanzania ameandika kuwa:

“Tanzania to the world! Anaitwa Ridley Asha Bateman 10, ni mtoto wa @rachel_luttrell (Zawadi), muigizaji mwenye asili ya Tanzania (Mama yake anatokea Tanga). Niliwahi kufanya makala yake pamoja na waigizaji wengine wa Hollywood wenye asili ya Tanzania.

“So, Ridley ameigiza kwenye filamu mpya ya Netflix inaitwa #Lou (ni kali sana nimeitazama wiki iliyopita). Ameigiza vizuri mno na hakika ana potential ya kuja kuwa tishio nchini Marekani. Pongezi nyingi sana kwa mama yake, Rachel kwa kumuongoza vyema bintiye katika career hii ya uigizaji.

“By the way, Lou ndio filamu namba moja kwa sasa Netflix. Waigizaji wengine ni @jurneesmollett, Logan Marshall-Green @elemgy na @allisonbjanney,” amesema Bundala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live