Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mfahamu bilionea mtoto, mali anazomiliki usipime

Muhammed Awal Mustapha1.jpeg Mfahamu bilionea mtoto, mali anazomiliki usipime

Tue, 9 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvulana mwenye umri wa miaka 10 kutoka Nigeria anaishi maisha ya kifahari mwenye magari makubwa, ndege ya kibinafsi na jumba la kifahari ambalo alipewa akiwa na umri wa miaka 6.

Muhammed Awal Mustapha, ambaye pia anajulikana Kama Mompha Junior, ni mtoto wa bilionea mashuhuri wa mtandao wa Nigeria Ismailia Mustapha, ambaye anajulikana kama Mompha, kulingana na ripoti.

Wakati Ismailia ana ufuasi wa zaidi ya milioni 1.1 kwenye Instagram, mtoto wake tayari amefikia idadi ya kuvutia ya wafuasi wa 26k na machapisho 9 pekee.

Katika picha kadhaa zilizopostiwa mitwndaoni, kijana ana onekana amevaa nguo za maridadi akiwa amesimama karibu na magari yake ya kifahari. Picha nyingine inamuonyesha akiwa na mlo ndani ya ndege binafsi.

Kulingana na ripoti ya The Sun, Mompha Sr. Ambaye ni baba yake, alimnunulia Mompha Jr. jumba lake la kwanza kwenye siku yake ya kuzaliwa akiwa na miaka sita mwaka wa 2018.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live