Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu Sam Mangwana, fundi wa muziki

Sam Mangwana Sam Mangwana.

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sam Mangwana alizaliwa mwaka 1945, Mama raia wa Angola na baba Mzimbabwe, alikulia Congo DR na kwa sasa anaishi Angola.

Alijulikana kwa jina la utani "Le pigeon Voyageur" maana yake ni njiwa anayesafiri, hii ni kutokana na tabia yake ya kutotulia sehemu moja.(Alikua akihama bendi moja kwenda nyingine na aliishi nchi mbalimbali.)

Mwangwana amebobea kwenye lugha, anazungumza kwa ufasaha idadi ya lugha ambazo utahitaji mikono miwili kuzihesabu, anazungumza kwa ufasaha Kilingala, kiswahili, kifaransa, kiingereza, spanish, kireno nk.

Umri wake ni zaidi ya miaka 70 ila hana mke. Hajawahi kuoa. Hana mtoto na hajawahi kuwa na mtoto/watoto.

Mangwana kajaliwa sauti nzuri na ni mmoja kati ya best vocalists nchini DRC. Unaweza kuthibitisha hili kwa nyimbo zake maarufu kama; Suzanne Coulibaly, Maria Tebbo, Fatimata, Bana ba Cameroon, nk.

Ni mmoja kati ya member wa bendi maarufu ya TP OK JAZZ BAND ambaye yupo hai, yeye pamoja na Wuta Mayi.

Amefanya kazi na bendi tofauti ikiwemo; African Fiesta( ilijulikana pia kama Afrisa International iliyokuwa inamilikiwa na Tabu Ley Rocherou), Los Batchichas, Negro Band, Orchestre Tembo, Festival Des Masquisards, TP OK JAZZ BAND, African All Star nk. Nami faida potea kama Kuna sehemu umesahaulika sawazisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live