Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu Neema Emmanuel anayeigiza sauti ya Gulfem

Wed, 2 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Akiwa na umri wa miaka 26, Sultan Suleyman alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottoman akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great.Utawala wake wa miaka 46 ulihitajika ulimwenguni kote akiwa na Pargali Ibrahim.

Kuhusu Gulfem Hatun

Huyu ni mke wa kwanza wa Sultan. Pamoja na kwamba Gulfem alizaa mtoto mmoja ambaye alifariki akiwa mdogo, ni mama ambaye si mkorofi.

Nafasi hii imechezwa na mtu anaitwa Selen Ozturk. Dada huyu aliyezaliwa miaka 28 iliyopita Izmir nchini Uturuki ni mwigizaji.

Mbali ya kuigiza kwenye Sultan, pia ameshaigiza kwenye tamthiliya nyingine ikiwemo Payitaht Abdulhamid, Hatirla Gonul na Benim Adim Gultepe.

Neema Emmanuel

Neema mbali ya kunakilisha sauti pia anafanya kazi ya kupamba kumbi za sherehe na kuremba mabibi harusi.

Wakati kwa upande wa kunakilisha sauti, anasema asingependa kuishia hapa kwa kuwa anaona kuna mambo mengi ya kufanya katika sanaa hiyo.

Kuhusu kazi gani hasa kati ya kunakilisha na kupamba inayomuingizia fedha, Neema anasema zote zinaingiza ijapokuwa zinatofautiana na watu unaofanya nao.

Kwa kazi ya kupamba ukumbi, anasema sehemu ambayo anaingalia zaidi ni pale anapokaa bibi na bwana harusi kwa kuwa ndio sehemu ambayo watu huitolea macho zaidi.

Anasema watu wanampenda Gulfem anajua sauti yake ni moja pia ya kitu ambacho kimewafanya wampende.



Chanzo: mwananchi.co.tz