Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu ‘Muno’ aliyemdatisha Rude Boy wa P Square kuja Tanzania

Asko Pic Data Mfahamu ‘Muno’ aliyemdatisha Rude Boy wa P Square kuja Tanzania

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Oviemuno Oriero maarufu Muno ni msanii  na mwandishi kutoka Nigeria ambaye Desemba mwaka huu amepanga kutembelea vyombo vya habari Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania.

Hatua hiyo  yake itaambaatana na listening party Pamoja na matukio mbalimbali,

Muno tayari amesharekodi ngoma kibao lakini pia ameshawahi kuwa chini ya labebo nyingi nchini Nigeria ikiwemo Lebo ya msanii Rude boy wa P Square inaitwa “Rude Boy Records”,

Wakati yupo Rude Boy Records, aliweza kuachia ngoma kama “Never regret” na baadae kushirikishwa kwenye ngoma ya “slow slow” ya Rude boy,

Kwasasa Muno yupo chini ya Management ya Champion on entertainment LTD , ambapo ametoa Ep yake mpya inaitwa 4+1 ambayo iliachiwa Septemba 17, mwaka huu .

Safari ya muziki ya Muno ilianza toka akiwa na umri wa miaka 10.

'‘Nilianza kuomba ruhusa na ujanja ujanja ili nitoke nyumbani na binamu zangu twende kwenye matamasha ili nikaimbe, na tulianzisha kundi na tukawa tuna perform kwenye matukio mbalimbali".

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz