Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu ‘Muno’ Chipukizi Aliyemkuna Rude Boy wa P Square

Oviemuno Oriero Oviemuno Oriero A.K.A Muno

Sat, 6 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Oviemuno Oriero A.K.A Muno ni Msanii na Mwandishi kutoka Nigeria Ambaye mwaka huu 2021 December Amepanga kufanya Media Tour yake Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania ,Media Tour yake itaambaatana na listening party Pamoja na Matukio mbalimbali.

Muno tayari amesharekodi ngoma kibao Lakini pia amesha wahi kuwa chini ya label nyingi nchini Nigeria ikiwemo Lebo ya msanii Rude boy wa P Square inaitwa “Rude Boy Records”.

Wakati yupo Rude Boy Records, aliweza kuachia ngoma kama “Never regret” na baadae kushirikishwa kwenye ngoma ya “slow slow” ya Rude boy.

Kwa sasa Muno yupo chini ya Management ya Champion on Entertainment LTD, ambapo ametoa Ep yake mpya inaitwa 4+1 ambayo iliachiwa September 17 mwaka huu 2021.

Safari ya muziki ya Muno ilianza toka akiwa na umri wa miaka 10 na kusema kuwa, "Nilianza kuomba dhuru na ujanja ujanja ili nitoke nyumbani na binamu zangu twende kwenye matamasha ili nikaimbe, na tulianzisha kundi na tukawa tuna perform kwenye matukio mbalimbali," amesema Muno.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live