Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu Cassie roboti anayekimbia sawa na Usain Bolt

Cassie Mfahamu Cassie roboti anayekimbia sawa na Usain Bolt

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Cassie ni roboti aliyetengenezwa kwa muda wa miaka mitano na watafiti wa uhandisi na mafunzo ya mashine (machine learning) katika Chuo Kikuu cha Oregon State na kampuni ya spinout, Roboti wepesi ili kuandaa njia ya ubunifu wa hali ya juu zaidi.

Roboti huyo ambaye watafiti wanasema anakichwa mfano wa mbuni alikimbia mita mia moja ndani ya sekunde 24.73, mda ambao bado hajaufikia wa Usain Bolt mwenye rekodi ya sekunde 9.58 ila kwa roboti kuweza kukimbia umbali huo bila kudondoka imeweka historia ya mafanikio makubwa kwao na kuishia kumuita Usain Bolt wa maroboti.

Katika riadha ya roboti huyo Cassie alikuwa amezungukwa na watu arobaini waliokuwa wakimshangilia pale tu akivuka mstari wa kumaliza mashindano, spidi na wepesi wa Cassie umeundwa na mafunzo ya akili bandia (Artificial intelligence), na hii imeonesha kuwa roboti wanaotembea kwa miguu miwili wana uwezo wa kuwa wajanja katika dunia halisi huku wakidumisha usawa, tatizo lililowakumba wabunifu wengi hapo zamani.

Maroboti wenye miguu miwili wamekuwa wakikumbana na matatizo kama kupoteza usawa (balance) na kuishia kudondoka chini, kwa miaka na miaka wanasayansi wamejaribu kutengeneza maroboti wa miguu miwili ambapo ndani ya mwaka 1960 watafiti wa Japan walitengeneza mifano ya mashine yenye miguu miwili, na hata wahandisi wa MIT na Chuo Kikuu cha California Institute of Technology wamejaribu kutengeneza, aidha kwa wiki iliyopita Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tesla alionesha kwa mara ya kwanza roboti mwenye mfano wa mwanadamu aitwaye Optimus.

Kutatua hilo tatizo, Fern alifanya kazi na Jonathan Hunt Profesa wa chuo kikuu cha Oregon State na pia muanzilishi wa Roboti wepesi ili kufundisha maroboti wanaotembea kwa miguu miwili kutumia akili bandia ( Artificial intelligence) na neva ya mtandao ambavyo ni algorithimu vya kuiga jinsi ubongo wa mwanadamu unavyofanya kazi.

Toka mwaka 2017 timu hiyo imekuwa ikimfundisha Cassie jinsi ya kutembea vizuri, kwa kutumia algorithimu kumpa zawadi roboti endapo akitembea vizuri, hii imeongozwa na saikolojia ya pavlovian, Fern akasema: "Anajifunza kwa kutarajia atapata zawadi na hivyo hufanya kitu kwa usahihi.”

Nancy J. Cooke, Profesa wa injia ya mfumo wa wanadamu Chuo Kikuu cha Arizona State alikumbusha kuwa marobiti wanazidi kuwa vizuri katika kufanya vitu kama kukimbia au kucheza mpira wa miguu, kipande kigumu ni kutengeneza maroboti ambao wataingiliana na wanadamu kwa njia ya asili Cooke amesema:

”Ambacho wanakosa ni utambuzi mgumu, bado kuna uelewa mkubwa wa wanadamu wa kukutana unaohitajika lakini hawana”

Cooke pia akaongezea kwa kusema kuwa maroboti kama Cassie wanazidi kuboreshwa katika viwanda vya kutengenza maroboti, lakini yaonesha hakuna haja ya kutengeneza maroboti ambao wanafanya vitu ambavyo wanadamu tayari wanaweza kufanya ni heri maroboti wanaofanya vitu asivyoweza mwanadamu wa kawaida kufanya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live