Nchi ya India ni kama sehemu nyingine Duniani ambapo kuna kumbwa na wimbi la umaskini, Huwenda ukawa ni mmoja ya waliokutana na mtu barabarani anayehitaji msaada kwa wapita njia kwa lugha tuliyoizoea ashakhum si matusi (omba omba).
Ulishawahi kuhisi kazi hii ya omba omba inaweza kumfanya mtu akawa tajiri kwenye hali ambayo mtu wa kawaida ngumu kuamini? basi wacha tukutaarifu kuhusiana na mwanaume mmoja huko nchini India.
Bharat Jain ambaye safari yake ya maisha ilikumbwa na changamoto nyingi kwenye kiwango cha wazazi wake kushindwa kumudu gharama za elimu ya awali, hii haikuwa kikwazo kwake kutengeneza ajira isyorasmi kwa ajili yake na familia yake.
Akiwa na utajiri unaotajwa kufikia Bilioni 2.4, Pesa ambazo amezipata kwa kazi yake ya omba omba, Inashangaza kidogo mh! makusanyo yake kwa mwezi ikitokea mwezi mbaya basi ukusanya mpaka kufikia Milioni 1,788,358.
Hatuna maana ya kuhalalisha hili, La! hasha kwani mbali na utajiri alionao kwa sasa ambao ni pamoja na Ghorofa na maduka mawili ya kupangisha tunaziita fremu huko Mumbai nchini India haijamzuia yeye kuendelea na kazi hiyo.
Tabia ni kama ngozi, ndio tuseme imekwisha kuwa sehemu ya maisha yake kwani cha kushangaza zaidi watoto wake wamefika elimu kwa kiwango kikubwa cha chuo na ni watu walio kwenye mfumo wa ajira hivyo maokoto mwisho wa mwezi sio kitu cha kuwaza kwao.