Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi ni mrahibu wa filamu

Messi 1832974123 Messi ni mrahibu wa filamu

Sat, 12 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kujiunga na klabu ya InterMiami kutokea nchini Marekani, Lionel Messi kwa sasa ameleta utofauti kwa mashabiki kila anaposhangilia goli.

Baada ya mchezo wa InterMiami dhidi ya Charlotte FC mchezo uliotamatika kwa Inter Miami kuibuka na ushindi wa goli 4 -0,

Lionel Messi alionekana akishangilia kwa ishara ya ''SPIDERMAN'' muhusika maarufu kwenye movie ya ''SpiderMan''

Hali iliyoibua hisia nyingi kwa mashabiki wa mpira wa miguu kwani imekuwa kama muendelezo kwa mchezaji huyu

Kwenye mchezo wa Inter Miami dhidi ya Atlanta United mchezo uliomalizika kwa Inter Miami kupata ushindi wa goli 4 - 1

Mchezaji Lionel Messi alionekana kwa mara nyingine akishangilia kwa ishara ya muhusika maarufu kwenye filamu ya ''The Avengers'' muhusika Thor (Mshika nyundo)

Kwenye mchezo wa Inter Miami dhidi ya Orlando City Mchezaji Lionel Messi alionekana akishangilia kwa mtindo wa filamu maarufu ya WAKANDA

Wapo wanaosema Messi anafanya hivyo kufurahisha watoto wake ambao huwa sehemu ya watazamaji wapo wanaosema Messi anafanya kuvutia mahusiano ya kibiashara na kampuni inayozalisha Filamu hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live