Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meneja wa Diamond athibitisha kukutwa na corona

99577 Salam++sk+pic Meneja wa Diamond athibitisha kukutwa na corona

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya uvumi kuzagaa tangu jana hatimaye meneja wa Diamond, Sallam SK amethibitisha  kuwa na ugonjwa wa corona. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sallam ameandika ujumbe akieleza kuhusu kuugua maradhi hayo. “Napenda kuwajulisha na kuwatoa hofu ndugu, jamaa na marafiki kuwa nimepata majibu ya vipimo na nimeonekana nikiwa na virusi vya corona. Kwa sasa nipo chini ya uangalizi na afya yangu inaendelea vizuri. “Pia niishukuru Serikali kwa maandalizi mazuri na huduma ninayopata wodini, kwenye kituo toka juzi nipo peke yangu kama nimekikodisha vile. Wahudumu wana ushirikiano mzuri, Mungu awalinde na awape afya njema maana wamejitolea nafasi zao kutupatia huduma sisi waathirika,” Sallam alitumia nafsi hiyo kutoa ushauri kwa kueleza kuwa “Hili janga la kimataifa linakwepeka kama tutafuata ushauri nasaha kutoka kwenye wizara husika naomba kwa wote tuwe salama na familia zetu, tuchukue tahadhari mapema,” Watu kadhaa wakiwemo wasanii wamesoma ujumbe huo na kuandika maneno ya kumpa faraja na kumtakia heri apone haraka.

Chanzo: mwananchi.co.tz