Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meja Kunta aingia kwenye soko la Kimataifa na Chuu

Meja Kunta Msd Meja Kunta aingia kwenye soko la Kimataifa na Chuu

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miezi michache tangu msanii wa Singeli Meja Kunta asaini na moja ya lebo kubwa hapa Tanzania Bxtra Records, nguli huyo wa muziki ameachia mkwaju wake mpya unaoitwa Chuu akiwa Baba Levo pamoja na Ntoshi Gazi.

Ntoshi Gazi sio jina jipya kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania kwani nguli huyo alishafanya kazi na wasanii wengine kutoka Tanzania ikiwemo Diamond Platnumz, Rayvanny na Whozu na sasa ameungana na Meja Kunta.

Kwenye Chuu Meja Kunta, Baba Levo na Ntoshi Gazzi wanaimba kuhusu bata na namna ya kuchangamka ukiwa kwenye starehe na ngoma hii ni project ya kwanza kutoka kwa msanii wa Singeli kushirikisha msanii kutokea Afrika Kusini.

Chuu imetayarishwa na Eyoo Kenny kutoka Tanzania na ni ngoma ya 4 kutoka kwa Meja Kunta kwa mwaka huu akiwa chini ya lebo ya Bxtra Records.

Kando na Chuu, kwa mwaka 2023, Meja Kunta alitoa ngoma tofauti tofauti ikiwemo Ushali, Demu Wangu Remix akiwa na Marioo pamoja na Tabia Mbaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live