Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meja Kunta achukizwa  na matapeli

Dcc4403aace9d1fa05dfcb438794d083 Meja Kunta achukizwa  na matapeli

Thu, 11 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa muziki wa miondoko ya singeli, Meja Kunta amechukizwa na baadhi ya watu wanaotumia majina ya wasanii kuomba misaada katika mitandao ya kijamii na kusababisha kuchafua majina yao.

Meja Kunta alitoa kauli hiyo baada ya kusambaa ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ukimwonesha msanii huyo akiomba msaada.

“Mnaanza kunishangaa na kuvunja uaminifu mnajua wazi nipo kwenye matatizo ina maana kisa msanii ndio nisisadiwe kweli naamini kauli ya tenda wema uende zako,” alisema Meja Kunta akielezea sehemu hiyo ya ujumbe iliyosambaamitandaoni yenye jina lake.

Kupitia ujumbe wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram, Meja Kunta alisema kitendo cha kutumia majina ya watu kuomba misaada ni kuchafuana na kushusha thamani ya mtu.

“Jamani mnaotumia mitandao kwa majina ya watu tunaomba mtumie vizuri ili kuunga mkono kazi zao, wale mnaotumia majina yao msitumie kuomba watu pesa na kuchafua kazi au thamani ya mtu sio vizuri mimi sina akaunti Facebook na sijaomba msaada wa aina yeyote hivyo epukeni matapeli,” alisema.

Kwa sasa Meja Kunta anafanya vizuri na wimbo wake unaokwenda kwa jina la Madanga ya Mke Wangu akiwa na D Voice.

Chanzo: habarileo.co.tz