Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meja Kunta: Sijui nilichelewa wapi kwa Tunda

Tunda Meja Meja Kunta: Sijui nilichelewa wapi kwa Tunda

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meja Kunta; ni staa wa muziki wa Singeli nchini Tanzania ambaye anafunguka kuwa, anajiuliza kipindi chote alikuwa wapi mpaka akashindwa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi mapema kabisa na mrembo Anna Kimario almaarufu Tunda?

Akizungumza, Meja Kunta anasema kuwa, hajawahi kufurahia mapenzi kama kipindi hiki ambacho yupo na Tunda.

Anasema kuwa, Tunda amemfanya kuwa mtu mwenye kipindi chote na kubwa zaidi amekuwa rafiki yake mkubwa.

“Yaani kiukweli nafurahia sana kuwa kwenye penzi hili mpaka najiuliza kabisa sijui hata nimechelewa wapi kuingia kwenye huba hili maana ni raha na niko na rafiki yangu ambaye tunaelewana sana,” anasema Meja Kunta ambaye penzi lake na Tunda kwa sasa limeshika kasi ya ajabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live