Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meek Mill akaangwa na Waafrika Twitter

Meek Mill, Rapa Meek Mill akaangwa na Waafrika Twitter

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa Meek Mill amejikuta akikaangwa na mashabiki zake toka barani Afrika kufuatia kauli yake tata kwenye mtandao wa X zamani Twitter, ambayo ilitafsiriwa kama dhihaka kwa Waafrika.

Meek Mill alikuwa kwenye Q&A ambapo aliuliza swali lake kwamba, “Do a lot of people play my music in South Africa I remember having on big show their [sic] few years back … how do yall listen to our music in South Africa???? On what platform or in Nigeria?” akimaanisha kwamba Watu wengi wanasikiliza Muziki wake barani Afrika, lakini Je, ni njia gani wanatumia kusikiliza Muziki? Akiliekeza swali kwa Afrika Kusini na Nigeria.

Sentensi hiyo ilipokelewa vibaya kwa Waafrika wengi kwenye mtandao huo wakihisi rapa huyo amewadhihaki kwa alichouliza kwani kumekuwa na Maendeleo makubwa ya Digital Platforms kama Spotify, iTunes, Apple Music, AudioMack, Boomplay na nyingine nyingi.

Mmoja aliandika “Hutegemea na msimu, kwenye Kiangazi huwa tunasikiliza muziki kupitia Mkonga wa Tembo, msimu wa Masika Twiga hunasa Signal na kupiga Muziki kwa sauti.”

Mwingine aliandika “Huwa tunawatuma ndege kuja Marekani kukariri hizo nyimbo halafu hurudi kutuimbia pindi tunapojikusanya kwenye mti wa Kijiji.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live