Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mediocre ya Alikiba ilikuwa fimbo kwa Diamond na Harmonize

DIAMOND ALIKIBA HARMONIZE.jpeg Mediocre ya Alikiba ilikuwa fimbo kwa Diamond na Harmonize

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna yule rafiki yako au adui yako yani hata umfanyie kitu gani ni ngumu sana kukuonyesha amekasirika na hata kulipiza kisasi.

Watu wa hivi unaweza ukawafanyia kila aina ya kero lakini amini nakwambia siku wakiamua kujibu mapigo utachemka.

Hiki ndio kilichotokea pale Alikiba, King wa Kariakoo alipoona kama wadogo zake Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz na Rajabu Kahali maarufu kama Harmonize wanaleta mazoea ya 'kiduanzi'

Kiba akaachia "Mediocre" ambayo iliwachana wawili hao kwa pamoja na ikawa ni kama funzo, sasa kama hukujua ni wapi aliwachana ngoja nikusanue kupitia mistari yake kwenye wimbo huo.

"Ushamba mwiko kwa mtoto wa Kariakoo, Sichezi na dada zangu nacheza na dada ako mixer mkong'oto, We unauza siso, mi ndio bishoo"

Hapa alichanwa bwana Diamond Platnumz

"Pru mpaka chini pigo, Unataka ‘U-KING’ wa mafundo, Mimi ndo baba kingdom, kingdom"

Hizi zilimwendea Konde Boy a.k.a Jeshi

Alafu mwisho akawachanganya wote

"Tena mnaji-show, huyu commando Stage mafundo, wachafu wa roho Waongeza zero"

Yani kiufupi ni kuwa King alichafukwa roho na ndio maana akawaambia "Mediocre" kwa kiswahili fasaha ni "Kawaida sana" yani hayo mnayoyafanya mimi nilishacheza nayo kitambo.

Basi ndo ikawa hivyo lakini yaliyopita si ndwele tugange yajayo si ndio?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live