Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mchungaji awataka wanawake kuwaombea michepuko wa waume zao

James Gh.jpeg Mchungaji awataka wanawake kuwaombea michepuko wa waume zao

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji anayezingirwa na utata James Ng’ang’a amewashauri washirika wa Kanisa lake la Neno Evangelism kuwaombea michepuko waume zao ili nao wapate wanaume wa kuwaoa.

Akihubiri katika ibada kanisani mwake hivi karibuni, Ng’ang’a aliwaambia wanawake walioolewa kuacha kuomba mabaya kuwapata hawara za waume zao, bali wanapaswa wawaombee nao pia waolewe.

"Naskia mnasema michepuko wafe. Wamama wanapenda hiyo sana. Sema bwana Yesu bariki mchepuko wa mume wangu, mpatie bwana wake," alisema pasta huyo.

Zaidi ya hayo, Ng'ang'a aliwatetea michepuko akisema, hawapaswi kulaumiwa kwani mara nyingi ni wanaume ndiyo huwavizia.

"Bwana yako ndiye mchepuko, ndiye anatanga tanga tanga. Basi kwanza ua bwana yako... Na umesema Yesu asifiwe, hatujaitwa kuua," aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live