Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mchungaji auawa na jirani kisa kuku

Mchungaji Auawa Na Jirani Kisa Kuku Mchungaji auawa na jirani kisa kuku

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji aliyetambulika kwa jina la Nick Davi mwenye umri wa miaka 46 ameuwawa kwa risasi baada ya kubishana na jirani yake kisa usumbufu wa kuku na mbwa kwenye nyumba moja waliopanga huko Las Vegas Marekani.

Polisi nchini Marekani wamesema kuwa Nick ameuwawa kwa risasi na jirani yake wa kike aitwaye Grace akiwa mbele ya familia yake baada ya mzozo wa muda mrefu juu ya usumbufu wa kuku na mbwa wa jirani yake huyo

Taarifa zinadai kuwa Nick alimshtaki Grace kwa baba mmiliki wa nyumba hiyo waliopanga juu ya kadhia za mbwa na kuku wa Grace jambo ambalo Grace hakulipenda

Wakati anatoka na gari akiwa na familia yake ndani Nick alizuiwa na gari ya Grace kwa mbele ndipo Nick aliposhuka na kuanza kujibishana na Grace ndipo Grace alipoamua kumpiga risasi.

Baada ya tukio hilo mke wa Nick alimkabili Grace na kufanikiwa kumpora bunduki huku wote wakibaki na majeraha mbalimbali.

Grace amefunguliwa kesi ya mauaji na kesi nyingine inayomkabiri ni kumiliki bastola kinyume cha sheria. Grace alitenda tukio hilo mwishoni mwa mwaka 2023

Chanzo: www.tanzaniaweb.live