Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mchungaji: Wenye ndoa fanyeni sana tendo la ndoa, ni kama divai

Tolu Odukoya Ijogun Tolu Odukoya-Ijogun

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji Tolu Odukoya-Ijogun ambaye ni mtoto wa kwanza wa mchungaji Bimbo Odukoya wa kanisa nchini Nigeria amewaambia wenye ndoa wafanye sana tendo la ndoa kadiri wawezavyo.

Anasema baba yake mzazi aliwahi kusema tendo la ndoa ni sawa na pesa usipoitumia nyumbani utaitumia kwingineko nje hivyo tumieni sana pesa (tendo la ndoa) nyumbani.

Mchungaji huyo ambaye ni mama wa watoto watatu amesisitiza kwamba tendo la ndoa ni sawa na mvinyo kadiri muda unavyoenda ndivyo linavyozidi kuwa tamu.

Ameyasema hayo wakati akitoa ushauri wa kindoa ikiwemo kuwaambia wanandoa wasipende kushindana wao kwa wao pia msameheane.

"Ukiwa katika ndoa fanya fanya tendo la ndoa mara nyingi. Wanandoa kutofanya tendo la ndoa ni hatari sana. Baba yangu aliwahi kusema tendo la ndoa ni kama fedha, usipoitumia nyumbani utaitumia kwingine’ Bwana na Bi, tumia pesa yako nyumbani. Ukweli: tendo la ndoa ni kama divai; inakuwa tamu zaidi kadri muda unavyokwenda.

“Ukiwa kwenye ndoa acha kushindana! Ndoa sio mashindano. Mafanikio yake ni mafanikio yako. Nyinyi wawili mmekusudiwa kukamilishana sio kushindana dhidi ya kila mmoja.

Ukiwa kwenye ndoa, samehe. Msamaha ni saratani, unahitaji kuichuna kabla haijaua penzi lako. Iwapo ni vigumu kusamehe.. mama yangu aliwahi kusema ‘Ndoa ni wasamehevu 2 wanaoishi pamoja’, alisema Tolu.











Chanzo: www.tanzaniaweb.live