Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mchungaji Mgogo acharuka vijana kuoa/kuolewa na wazee

Mgogo Oneee Mchungaji Mgogo

Fri, 9 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji maarufu nchini Tanzania, Daniel Mgogo amecharukia suala la vijana wadogo kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na wazee waliowazidi umri maradufu.

Mchungaji Mgogo amewazomea vijana hao na kuwataka kujiepusha na mitego kama hiyo kwani tabia hiyo ni kama kushiriki katika kula mali ya babu yako aliyetangulia mbele ya haki kitambo.

Mgogo pia hakuwasaza wakongwe hao wanaojiingiza katika mapenzi ya vijana wadogo, wake kwa waume akiwataka kujiheshimu na kukoma kuwapotosha vijana kwani kanisa linataka vijana wengi kufanya harusi na vijana wenzao ili kukuza kizazi kijacho.

Mgogo akionesha kuchukizwa, alipinga vikali dhana kwamba umri ni namba tu na kusema kwamab hakuna vile vijana wanaweza ingia katika mapenzi na wazee na mahusiano hayo kutarajia kupata watoto wa kuendeleza kizazi cha usoni.

“Kijana mbichi anajihusisha kimapenzi na jimama. Baba zake walijishughulisha naye ana hili baba zake walizaa watoto na huyu mama na wewe unaenda, utazaa watoto na huyu ana miaka sabini. Alafu mnatuambia, umri namba. Vijana tunategemea waoe tufunge harusi, watuletee wajukuu. Watu wanasukumana na mabibi minyanya,” Mchungaji Mgogo alitema moto.

Anawakashfu vijana wengi siku hizi ambao wanatebwereka na kusubiria embe kudondoka kutoka mtini pasi na kufanya juhudi zozote za kukwea ili kulichuma lile embe kwa nguvu zao.

Kwa mujibu wa Mgogo, vijana hao wanafanya kula mali za babu zao jambo ambalo amechukizwa nalo.

“Kweli kijana mdogo jitegemee, unataka kula mali za babu yako aliyekufa alimuacha huyu bibi. Wachana na huyo mama! Nenda tafuta size yako tunataka watoto,” Mgogo anasisitiza.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na matukio yasiyo ya kawaida ambapo unawapata vijana wadogo wanajihusisha katika mahusiano ya kimapenzi na ajuza na babu waliopitwa na umri na unapata baadhi ya watu wanashabikia mahusiano hayo, jambo ambalo kwa mchunaji Mgogo si kitu cha kufurahisha bali kukemewa vikali kwa sababu wengi wakilikumbatia, basi kizazi cha kesho hakimo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live