Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchengerwa aagiza oparesheni waharamia

IMG 20221019 WA0014 768x576 Mchengerwa aagiza oparesheni waharamia

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameiagiza Ofisi ya Hakimiliki Tanzania kukamilisha marekebisho ya Sheria ya Hakimiliki katika eneo la uharamia pamoja na Kanuni kabla ya tarehe 01/11/2022 na kufanya operesheni ya uharamia.

Mheshimiwa Mchengerwa ametoa agizo hilo jana Oktoba 18, 2022 Jijini Dar es Salaam katika kikao chake na viongozi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania na Azam Media Ltd kufuatia malalamiko ya Kampuni hizo ya wizi wa maudhui.

“Suala la uharamia nafahamu kuwa limekithiri, Ofisi ya Hakimiliki toeni elimu kwa wadau na toeni matamko ya kukemea uharamia,” alisema Mhe.Mchengerwa.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho, Waziri huyo alisisitiza kuunda Kamati ya uharamia hivi karibuni ambayo itadhibiti uharamia.

Naye Muwakilishi wa Msimamizi wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania, Bw. Baraka Katemba alifafanua kuwa tayari Ofisi hiyo imeshandaa Kanuni hizo ambazo kama ilivyoelekezwa na Maboresho ya Sheria yanaendelea kufanyiwa kazi na ameahidi kuwa maelekezo yote yaliyotolewa yatakamilika kwa wakati.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Multichoice Tanzania alieleza namna Kampuni hiyo inapata hasara kutokana na Uharamia wa maudhui wanayozalisha kutokana na baadhi ya wadau kurusha maudhui hayo bila kibali chao, pia alieleza namna Serikali inakosa mapato kutokana na baadhi ya wadau kutumia ving’amuzi ambavyo wanaviingiza kimagendo na kuvitumia kurusha matangazo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live