Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchekeshaji achangisha pesa za msaada wa dola milioni 1.6 saa 48

Mchekeshaji Achangisha Pesa Za Msaada Wa Dola Milioni 1.6 Saa 48 Mchekeshaji achangisha pesa za msaada wa dola milioni 1.6 saa 48

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Kampeni ya umma inayoungw amkono na mchekeshaji wa Ethiopia Eshetu Melese imepelekea kuchangishwa kwa kiasi cha dola milioni 1.35 katika kipindi cha saa 48 kwa ajili ya msaada ambao unalenga kujenga kile kilichoelezewa kama makazi ya kwanza kwa ajili ya watu wasio na makazi nchini Ethiopia.

Pesa hizo zimepatikana kutoka kwa wahisani 15,200, huku kiwango cha juu cha msaada kikiwa ni $10,000.

Kampeni ya GoFundMe inalenga kusaidia shirika la msaada la Mekedonia.

"Fanya mabadiliko katika maisha ya wakongwe wasiohesabika na watu wenye changamoto za kiakili wanaoishi katika hali mbaya katika mitaa – tusaidie tujenge nyumba kwa ajili ya wasio na nyumba ,"inasema.

TMchekeshaji huyo pia alilisaidia shirika hilo kuchangisha misaada kutoka katika benki nchini humo, licha ya kwamba kiwango hicho cha fedha hakiko wazi.

Eshetu ni msanii kijana wa vichekesho na muandalizi wa kipindi cha TV nchini Ethiopia . Amekuwa maarufu katika miak aya hivi karibuni kwa kipindi ambacho kinawahusisha watoto wenye vipaji.

Kampeni za aina hiyo hutegemea kwa kiasi kikubwa misaada kutoka kwa idadi kubwa ya Waethiopiawaishio nje yan chi – hususan Marekanina Ulaya – na wanaonekana kujitolea kwa ajili ya shughuli hiyo.

"La muhimu sio ukubwa wa zawadi bali ni ukubwa wa moyo," unasema ukurasa wa uchangishaji.

Chanzo: Bbc