Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mch. Mashimo: Ostaz Juma ana stress za maisha, asipambane na Diamond

MASHIMO JUMA NAMUSOMA Mchungaji Mashimo, Ostaz Juma na Diamond

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhubiri Maarufu jijini Dar es Salaam, Mchungaji Daud Mashimo amemvaa aliyewahi kuwa mejena wa wasanii mbalimbali na mdau mkubwa wa masuala ya muziki nchini, Ostaz Juma Namusoma kutokana na kauli za jamaa huyo kumshambulia msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

Mashimbo ameibuka baada ya Ostaz Juma kumponda Barnaba kwa kupiga picha na Diamond na kukubali kushirikiana naye kimuziki akidai kuwa nyota yake imechukuliwa na huo ndiyo mwisho wa umaarufu wake kwenye game ya muziki.

“Ostaz Juma Namusoma ni mganga wa kienyeji tu, kwanza ni mnyanyasaji wa kijinsia, kitendo alichomfanyia Dogo Janja mimi kilikiera ndiyo maana Mungu alimshusha, hatoweza kuinuka tena.

“Alimpigisha magoti Dogo Janja na PNC, kwa ukatitri huo watu msimwamini, ana stress za maisha, bora aje hata kwangu awe anasafisha viatu ama gari yangu, nitamlipa.

“Ostaz Juma ana nini? Hana kitu, kutoka kuwa mwandaajia, mfadhiri mpaka kuja kuwa mshangiliaji, hana lolote. Asipambane na Diamond hawezi kufika viwango vya Diamond. Mpaka sasa hana nyumba hapa mjini.

“Anasema ameumia kuona Barnaba amepiga picha na Diamond, mimi nimuulize Ostaz Juma yeye alipiga picha na Diamond? Mbona amefuria? Mbona ameishiwa? Hana kichwa wala mbele… Huyu ana stress za maisha.

“Kazi ya Diamond ni kuzalisha na kuinua vipaji, yeye (Ostaz) wasanii wawili tu walimshinda, PNC na Dogo Janja, mpaka akawatesa na kuwanyanyasa. Sasa atujibu, nyota yake imekufa, na yeye kufuria, kama kila mtu akipiga picha na Diamond anakwisha, je alipiga picha na Diamond?

“Wimbo wa ‘Kanyaga’ wa Diamond umemkera kwa sababu ulikanyaga mafisadi na wanafiki kama yeye, kufufua mambo ili kuchonganisha watu. Ostaz Juma namjua vizuri, alikuwa akiishi nyumba ya kupanga nyuma ya Stendi ya Magufuli (Mbezi Luis) na alikuwa akilipa shilini 150,000 tu kwa mwezi, lakini Diamond analipa shilingi milioni 42 kwa mwaka.

“Sasa yeye mlo wake kwa siku Ostaz Juma ni shilingi ngapi? Anasingizia mfungo kumbe hana hela. Atuonyeshe mafanikio yake. Huyu ni mnafiki, ana chuki binafsi. Leo anapambana na Diamond, toka lini masikini akapambana na tajiri? Muulizeni anaishi wapi? Asimseme vibaya Diamond.

“Alichofanya Diamond ni kuwainua wasanii kama Harmoinize, Rayvanny na wengine, sasa ni zamu ya Barnaba, ni zamu ya Aslay kuinuliwa, wasimuonee kinyongo Diamond, ni mzazi, anazaa vipaji. Huu ndio wakati wa Barnaba,” amesema Mchungaji Mashimo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live