Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbwa atafuna Sh milioni 10 za ujenzi

Mbwaaaa (17).jpeg Mbwa atafuna milioni 10 za ujenzi

Fri, 5 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbwa aitwaye Cecil anayemilikiwa na Clayton Law na Mkewe Carrie Law ambao ni Wakazi wa Pittsburgh nchini Marekani ameibua gumzo baada ya kuichanachana bahasha iliyokuwa na dola elfu nne za Kimarekani (USD 4000) na kuzitafuta pesa zote.

Wanandoa hao licha ya kupata hasira na hasara ambayo inafikia milioni 10 kwa pesa za Kitanzania, wameendelea kumsifu mbwa huyo kuwa ni mpole na hii ndio mara yake ya kwanza kutafuna pesa zao, kuzichanachana huku wakiamini amemeza zaidi ya dola elfu mbili.

“Cecil alikuwa mbwa mbaya siku ya kwanza tulichukia lakini kwa sasa tunacheka tu tukiwaza hili tukio, zimepita wiki nne tangu tukio litokee na tunashukuru mbwa wetu anaendelea vizuri hajaugua na ameendelea kuwa mbwa mzuri kwetu” ——— wamesema Wanandoa hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live