Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Mbunge ataka wanaume wanaonyimwa unyumba wazungumze

5df42d15946e9cfc27f731da5faa707b Mbunge ataka wanaume wanaonyimwa unyumba wazungumze

Sun, 6 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MBUNGE wa Jimbo la Nkasi Kaskazini mkoani Rukwa, Aida Khenani (Chadema) amewashauri wanaume mkoani humo wanaopigwa au kunyimwa unyumba na wenza wao wasione aibu na kunyamaza bali wazungumze ili wasaidiwe.

Alisisitiza kuwa visa vya kupigwa na kunyimwa unyumba na wenza wao ni ukatili huku akiwataka wasiogope bali wawe jasiri kuvunja ukimya vinginevyo wataendelea kuteseka kimya kimya.

"Wawe na ujasiri kama tulivyo sisi wanawake tumevunja ukimya kwa kupaza sauti zetu.......ukatili ni ukatili hata mwanamke anapompiga mwenza wake wa kiume ni ukatili vivyo hivyo kwa mwanaume,"a lisisitiza.

Alitoa ushauri huo katika mahojiano na HabariLEO wakati dunia ikiwa katika mfululizo wa siku 16 za kuhamasisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia huku akikiri kuwepo kwa visa vya wanawake kuwafanyia ukatili wa kijinsia wenza wao wa kiume mkoani humo.

Alitoa rai kwa wanawake kuwa hata kama wamefanikiwa kimaisha waendelee kuwaheshimu waume zao bila kiburi vivyo hivyo kwa wanaume..

Baadhi ya wanaume waliohojiwa na gazeti hili kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini wamekiri kuwa wapo baadhi yao wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia na wenzao wao.

Walikiri kuwa pia baadhi ya watumishi wa umma wanakumbwa na kadhia hiyo ya kupigwa na wake zao na hawasemi wanaumia kimya kimya.

Huku baadhi ya watoto wakipaza sauti zao wakieleza kutofurahishwa kwao na ukatili wanaofanyiwa na baadhi ya wazazi na walezi nyumbani

Chanzo: habarileo.co.tz