Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge 'Jah People' afunga ndoa, kula na kunywa bure!

Deo Sanga Mbunge 'Jah People' afunga ndoa, kula na kunywa bure!

Wed, 14 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Makambako Mkoani Njombe Deo Sanga maarufu kwa jina la Jah People amefunga ndoa na Mpenzi wake wa muda mrefu Rozana Kapasi.

Ibada imefanyika leo katika Kanisa Katoliki Parokia Mtakatifu Paulo Ilangamoto lililopo Mjini Makambako na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo kwa niaba ya Rais Samia.

Mbunge Sanga amefanya sherehe kubwa katika uwanja wa mpira wa miguu wa Amani huku Wananchi wakiingia bure katika uwanja huo na kusherehekea ndoa hiyo kwa kula na kunywa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live