Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbosso funguka kuhusu mtoto wake

Mon, 16 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwanamuziki wa kundi la WCB,  Mboso Khan amesema ipo siku familia ya mzazi mwenzake, Boss Martha itaona umuhimu wa kujadili kuhusu mtoto wake.

Mboso ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Septemba 14, 2019 wakati akizungumza na Mwananchi ikiwa ni siku moja baada ya mazishi ya Martha, msanii wa kundi la vichekesho la Cheka Tu  ambaye Mbosso anasema amezaa naye mtoto.

“Nimeshiriki mazishi na familia ya Martha,  isingeweza kunizuia  kwa sababu inafahamu nini kinaendelea kati yangu na yeye. Kitendo cha kunikana si kipya na nilitarajia watafanya hivyo kwa sababu walishanikana siku nyingi,” amesema Mbosso.

Amesema lengo lake si kumdai mtoto bali kueleza siri yake na Martha kuhusu kutoweka wazi suala la mahusiano yao, mtoto.

“Chochote nitakachofanya sasa nitaonekana ninafanya fujo, ndio maana nimeacha ili Martha niliyekuwa ninampenda sana apumzike kwa amani.”

“Hakuna mzazi anayemchukia mwanaye, ninajua ipo siku familia ya Martha itanipa mtoto wangu Ibrahim ambaye wao wanamuita Joseph,” amesema Mbosso.

Pia Soma

Advertisement
Ameongeza, “Nilikuwa naletewa mara kwenye gari, siku nyingine nyumbani kwa Martha na wakati mwingine kwa rafiki zake. Anajua kuwa mimi ni baba yake nina imani siku moja tutakuwa pamoja akiniita baba na mimi nikimuita mwanangu.”

Chanzo: mwananchi.co.tz