Msanii wa WCB Mbosso amehoji tuzo za ‘Tanzania Music Awards’ baada ya kutolewa washiriki na vipengele vya tuzo hizo akisema zina lengo kuwatunza watu ambao kamati inaweza kuwamudu.
Kupitia Insta Story yake Mbosso ameandika “Tatizo la tuzo za Tanzania zinalengaga kuwatunza watu ambao kamati wanaweza kuwamudu, kuwaendesha na kuwatumikia watakavyo na sio waliofanya kweli vizuri ki uhaki”.
“Labda pengine mie zumbukuku Kilungi, mniambie nyie ‘Khan EP’ ilikuwa na kigezo gani cha kutokuwepo kwenye Album/EP bora? halafu mniambie hizo zilizokuwepo zilitoa hit ngapi maana Khan EP imetoa Huyu Hapa, Shetani, Yataniua na Assalam nyimbo ambazo zimesumbua sana nyumba, mitaa, club na hata waliotoa Album pamoja nami zote Album zao zilizima.
“Tatizo kamati mnaendekezana sana roho mbaya na chuki, sasa hivi naelewa kwanini wasanii wenye kuijua thamani yao hawataki kushiriki”.
Aidha, BASATA nao wametoa taarifa inayoeleza kuwa msanii mwenyewe kwa hiari yake ndio anaweza kuweka kazi zake kwenye vipengele vya tuzo ambavyo amejiridhisha.