Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbosso aonesha mahaba kwa Uwoya, amkataa Tuerny

UWOYA MBOSSO Mbosso aonesha mahaba kwa Uwoya, amkataa Tuerny

Tue, 2 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbwana Kilungi aka Mbosso ameweka wazi kuwa endapo akiwekewa warembo wawili, muigizaji Irene Uwoya na soshaliti Tuerny mbele yake chaguo lake la kwanza litakuwa ni Uwoya.

Mbosso amefunguka hayo Jumapili iliyopita alipokuwa kwenye kipindi cha BIG Sunday kinachorushwa na Wasafi TV ambapo alipoulizwa ni yupi anamchagua kati ya wawili hao ndipo aliposema Uwoya ndio chaguo lake la kwanza.

Alisema, sababu za kumchagua Uwoya ni kwamba ni mrembo ambaye amekuwa hivyo miaka mingi tofauti na warembo wengine.

“Nitamchagua Uwoya maana kwa kweli hachuji, Uwoya tangu kipindi cha filamu ya Oprah yupo hivi hivi tu hajawahi kubadilika,” alisema Mbosso.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live