Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbosso: Rich Mavoko ameweka alama kwenye maisha yangu

Mavokooo Mbossooo Mbosso na Mavoko

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya WCB Wasafi, Mbwana Yusuph Kilungi maarufu kama Mbosso ameanika wazi kuwa msanii mwezake Rich Mavoko ni miongoni mwa watu ambao wana alama kubwa kwenye maisha yake ya muziki wake.

Mbosso amesema hayo kupitia kipindi cha Big Sunday Live ya Wasafi TV na kuonesha umhimu wa Mavoko katika maisha yake.

"Mavoko ni mtu ambaye tulikua tanakaa pamoja mtaani Tabata, kipindi natakiwa niingie Wasafi mimi nilikua nimeacha masuala ya muziki kabisa nilikua nacheza tu mpira Tabata.

“Kwa hiyo wakati nachukuliwa WCB, nakumbuka Mavoko ndio alikuwa anakuja home kunichukua kwenye gari yake tunaenda Wasafi halafu tunarudi wote nyumbani, yani ni mchizi ambae kwa kiasi flani ana alama kwenye maisha yangu ya muziki," amesema Mbosso.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live