Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbosso: Otile Brown hana madhara kwangu

Brown Mbosso Mbosso na Otile Brown.

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bifu linalotokata chini ya maji kama inavyosemekana kati ya msanii kutoka WCB Wasafi, Mbosso pamoja na msanii kutoka humu nchini Kenya Otile Brown.

Mbosso aizungumza kwa mara ya kwanza kupitia mahojiano na kituo cha radio Tanzania kwamba hana tatizo na Otile wala msanii yoyote yule kwani anakwepa sana mambo hayo japo Otile ashawai kusema ashaibiwa wimbo.

Mbosso amesema kuwa hana ushikaji na Otile japo kuna wakati Otile alidai kolabo lakini akashindwa mwenyewe kutokana na taratibu zilizoko.

Ikumbukwe kwamba Mbosso yuko chini ya uongozi wa WCB, kufanya kazi na yeye lazima upitie taratibu fulani jambo ambalo Otile ni kama hakulichukulia poa na huenda ikawa ndiyo chanzo cha wawili hao kutokua na ushikaji.

Hata hivo Mbosso amedai kuwa, Otile hana madhara yoyote kwake kwani hajafikia ukubwa huo;

"Sina tatizo na Otile wala msanii yoyote mimi nataka muziki tu, ameshawahi nicheki akitaka kolabo ila nikampa utaratibu, naona alishindwa mwenyewe kwa sababu niko chini ya uongozi.

"Kwa hiyo kufanya kazi na mimi lazma ufate taratibu zinazotakiwa, halafu hana madhara kwangu hajawa na hiyo nguvu, kwa hiyio poa tu," amesema Mbosso Khan.

Je, ni kweli Otile hajafikia ukubwa wa kumbabaisha Mbosso?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live