Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbosso: Nafikiria kuachana na muziki

Mbosso: Napenda Kuigiza, Nipeni Dili Mbosso: Nafikiria kuachana na muziki

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Mbwana Yusuf Kilungi, maarufu kama Mbosso Khan amesema kuwa, hafikirii kufanya kazi za muziki katika maisha yake yote bali anafikiria kustaafu ili aishi maisha ya kawaida.

Mbosso amesema hayo wakati akihojiwa na PLANET BONGO YA EAST AFRICA RADIO huku akisema muziki sio kitu ambacho atakifanya muda wote wa maisha yake.

“Kuna stage ikifika nitasema hapa inanitosha, sina makadilio ya mwaka kwa sababu nikisema naweka baada ya miaka kadhaa, Mungu anaweza kunichukua kesho, kwa hiyo kuna muda najipa ambao najua utanitosheleza.

“Natakiwa nikae kijamii, hapa nishiriki vitu vingine, nahitaji kukaa kwenye maisha mengine tofauti na muziki. Muziki ni kitu kizuri sana, ni kipaji Mungu anakupa unapata riziki lakini ndani ya muziki kuna vitu vingi ambavyo mashabiki hawavijui, kuna chuki, vita, roho mbaya, kifupi ni mambo mengi yako ndani yake.

“Binafsi ulimwengu huo unanitesa sana, ndiyo maana nataka nifanye muziki wangu kwenye njia yangu, sio mambo ya kuniongelea bali mtu anijue kupitia muziki wangu na si vitu vingine, muda ukifika nitasema hapa nimetosha napumzika muziki,” amesema Mbosso.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live