Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Mbinu za kumfunga breki mwanaume anayesaliti penzi

Wapenzi Couple.png Mbinu za kumfunga breki mwanaume anayesaliti penzi

Thu, 3 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hofu kubwa anayoweza kuwa nayo mwanamke aliye katika ndoa, au katika uhusiano wa kudumu, ni mumewe au mpenzi wake kumsaliti kwa kutoka na mwanamke mwingine!

Wengi hubaki na hofu kubwa ndani ya mioyo yao kwamba itakuwaje kama mume au mpenzi atanogewa na utamu wa penzi la mchepuko?

Sasa kama wanawake wengi wanahofia kuwapoteza wanaume wanaowapenda, ni wangapi wanajua wanatakiwa kufanya nini ili ndoa ziendelee kudumu, mapenzi yaendelee kuwa matamu na uaminifu uzidi kudumu katika ndoa?

Utashangaa kugundua kwamba wengi hawajui nini wanatakiwa kukifanya ili waendelee kujihakikishia nafasi kwenye ndoa au uhusiano waliopo, matokeo yake wanakuwa wanabahatisha tu.

1.KAULI NZURI Mwanasaikolojia mmoja nchini Uingereza, amewahi kueleza kwamba mwanamke anapokosa kauli nzuri ndani ya nyumba, akawa ni mtu wa kuongea hovyo, kufoka au kutukana, picha inayomjia mwanaume akilini mwake, ni mama mkali anavyomfokea mwanaye na wakati mwingine kumuadhibu.

Yaani ukiwa na kauli za hovyohovyo kwa mumeo, hatakuona kama mkewe, atakuona kama mama wa kambo mwenye roho mbaya ambaye kazi yako ni kumuwazia mabaya au kuunda njama za kumkomoa.

2.UWAZI NA UAMINIFU Silaha nyingine kubwa inayoweza kumfanya mwanaume asifikirie kabisa kukusaliti na ajivunie kuwa na wewe, ni kuwa muwazi na mwanimifu kwake.

Ukiwa na tabia ya aina hii, maana yake kuna mambo mengi unayomficha mwenzi wako na ndiyo maana huwezi kumpa simu yako akakaa nayo hata kwa dakika moja. Ukitaka mume akuheshimu, anza kwanza kujiheshimu wewe mwenyewe, acha mazoea yasiyofaa na watu wa jinsia nyingine...Itaendelea wiki ijayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live