Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mbinu ya kusikiliza voice note WhatsApp bila watu kusikia

Mbinu Ya Kusikiliza Voice Note WhatsApp Bila Watu Kusikia Mbinu ya kusikiliza voice note WhatsApp bila watu kusikia

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wapo baadhi ya watumiaji wa mtandao wa WhatsApp wamekuwa wakipata shida kusikiliza Voice Note wanazotumiwa wakiwa mbele za watu kwa kuhofia jumbe zao kusikiwa na watu wa pembeni, bila ya kufahamu kuwa ipo njia nyepesi ya kusikiliza Voice Note bila ya walio pembeni kusikia kitu.

Mtumiaji wa WhatsApp endapo utatumiwa ujumbe kwa njia ya Voice Note ukiwa mbele za watu na hauna Ear Phones, bado una nafasi ya kusikiliza ulichotumiwa bila ya wengine kusikia kitu.

Unachotakiwa kufanya ni kufungua sauti uliyotumiwa na kisha kuweka simu sikioni kama unazungumza na mtu, kwa kufaya hivyo sauti unayosikiliza haitafika kwa watu wengine badala yake itasikika tu kwenye spika ya mbele na utaisikia wewe pekeyako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live