Msanii Mb Doggy (@mbdogg_master) ametoboa siri kuwa Wimbo wake uliopendwa na wengi wa Mapenzi kitu gani sio hata wimbo wa mapenzi kama inavyodhaniwa bali aliutunga ili kushukuru vyombo vya habari vya kipindi hicho kwa kusapoti mziki wake.
Kwenye shairi lifuatalo amevitaja vyombo vya habari (Radio) kadhaa kama ifuatavyo:-
"Uamini MIUJIZA mchumba Sauti ya NYUKI inasikika Sogea karibu Baby TIMES zishafika Unipe UHURU Dear ni-KISS ninapotoka, toka MLIMANI Dear niwe FREE ndani ya kopa. Penzi kwa fujo My Buba Moyo wangu ushauteka, Raha ya Africa RTD mimi ndo hewani nasikika, hivi kwanini Dear moyo wangu unautesa, Hivi hushoboki Dear inavyonipenda EAST AFRICA.