Floyd Mayweather anaripotiwa katika harakati za kununua nyumba 1000 za bei nafuu, zinazojumuisha majengo 60 kwa Dolla za Kimarekani 402 milioni ambayo ni zaidi ya shilingi Trillion 1 kwa pesa ya Kitanzania kwa mujibu wa kampuni inayojihusisha na uuzaji wa nyumba nchini Marekani iitwayo Real Deal.
Mali hio inaweza kuhudumia familia nyingi, ambayo kimsingi iko Manhattan na imepelekea hii kuwa moja ya mpango mkubwa zaidi wa mali isiyohamishika huko New York mwaka huu.
Chanzo kinaripoti kuwa sehemu ya malipo imefanyika Jumatano na malipo mengine yanatarajiwa kufungwa mwishoni mwa 2024 au mapema 2025.
Nae Floyd Mayweather Jr amesema; "Ununuzi huo una umuhimu mkubwa wa kihisia kwangu na kwa familia yangu"