Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawe ya Wagosi wa Kaya yalimfanya Rais Mkapa anunue albamu ya 'Ukweli Mtupu'

Bao Full Wagosi Mawe ya Wagosi wa Kaya yalimfanya Rais Mkapa anunue albamu ya 'Ukweli Mtupu'

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unajisikiaje baada ya kufanya kazi kubwa ya kuikosoa Serikali, nondo kwa nondo, halafu unaambiwa, Mkuu wa Serikali anapenda kazi yako?

Iliwatokea Wagosi wa Kaya. Mwaka 2002, waliingiza sokoni albamu yao ya kwanza “Ukweli Mtupu”. Ilikuwa albamu ya kishujaa kwa wananchi. Waliogongwa waliwaona Wagosi, wanoko.

Zile nondo “Tanga Kunani”, yale mawe “Wauguzi”, ule mfatuma wa umeme na maji kwenye “Kero”, ile shubiri ya majungu kazini katika “Vinatia Uchungu”, lile darasa pilipili la “Mkulima”. Wagosi walipiga uppercut nyuzi 360.

Watanzania waliipokea Ukweli Mtupu kwa upendo, wakainunua kwa fujo. CEO wa MJ Records, Master Jay na Wagosi wenyewe, mikono ilivimba kwa kugonga kopi. Usiku walikesha wanaweka mihuri, mchana wanaambiwa zimeisha, wagonge nyingine.

Wanaa hawakuwaacha Wagosi wale hela za jasho lao peacefully. Vitisho vilitoka ndani ya system hadi kwa wapambe wa viongozi. Wagosi waliambiwa wanatumiwa na wapinzani kuisema Serikali. Eti, wangekiona cha mtemakuni.

Yusuf Makamba, by de facto, ndiye King wa Wagosi wote. Wakati huo, Makamba alikuwa RC wa Dar es Salaam.

Ruge Mutahaba ni undeniably behemoth wa game ya Bongo Flava. Alinyanyua simu moja kwa Wagosi: “Kuna sehemu inabidi niwapeleke.” Umba ile sauti yake kama inatokea puani.

Hodi hodi mpaka ndani, nyumbani kwa Makamba. Ruge na mijitu miwili, Dr John na Genius Mkoloni “Wagosi wa Kaya”.

“Mzee, wale vijana wako ndio hawa hapa,” Ruge aliwatambulisha Wagosi kwa King wa Wagosi.

“Oooh, ndio ninyi. Nawasikia tu.” Umba ile sauti yenye lafudhi ya Kigosi. Halafu akawashangaza: “Rais Mkapa anapenda muziki wenu. Anafurahia ujumbe mnaoutoa. Amenunua albamu yetu. Anatembea nayo kwenye gari. Kila wakati anawaisikiliza.”

Wagosi walidata. Raia Namba Moja, anapenda kazi yao, waliokuwa wanawatisha, waliowaona visisimizi. Wakarejea studio, wakaunda albamu “Ripoti Kamili”, nayo ilijaa visanga si kitoto.

Kama Rais Mkapa aliwakubali, wewe nani upinge Wagosi kutunukiwa hadhi maalum ya Bongo Flava Honors?

Tukutane Oktoba 27 (Ijumaa hii), Alliance Francaise, Upanga. Sugu The Jongwe ataongoza tukio. Halafu ni shoo-shoo kwa live band.

Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live