Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawaziri wahudhuria shindano la Miss Tanzania

16406 Miss+Tanzania+pic TanzaniaWeb

Sun, 9 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shindano la Miss Tanzania 2018 linafanyika usiku wa leo Jumamosi Septemba 8,  2018  na miongoni mwa waliohudhuria ni Waziri wa Habari,  Utamaduni,  Sanaa na Michezo,  Dk Harrison Mwakyembe pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Japhet Hasunga.

Wengine ni mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,  Jokate Mwegelo na  Miss Tanzania mwaka 2004,  Faraja Kota.

Tayari washiriki wa shindano hilo linalofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) wameshapita raundi ya kwanza na kujitambulisha wakijiandaa kupita mbele ya mamia ya waliohudhuria shindano hilo,  wakiwa wamevalia vazi la ubunifu.

Washereshaji katika  shindano hilo ni mwanamitindo Hamisa Mobeto na mtangazaji wa kituo cha runinga cha EATV, Deogratius Kitham

Chanzo: mwananchi.co.tz