Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawakili wa Babu Tale waibua utata

Babu Tale Kwa Koti.jpeg Mawakili wa Babu Tale waibua utata

Sun, 11 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mawakili wa meneja wa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva), Abdul Nassib ‘Diamond Platnumz’, Hamisi Shaban Taletale, maarufu kama Babu Tale wameshindwa kufika mahakamani mara mbili kuhudhuria kesi za mteja wao huyo ambaye yuko hatarini kufungwa huku wakitoa maelezo tata.

Dar es Salaam. Mawakili wa meneja wa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva), Abdul Nassib ‘Diamond Platnumz’, Hamisi Shaban Taletale, maarufu kama Babu Tale wameshindwa kufika mahakamani mara mbili kuhudhuria kesi za mteja wao huyo ambaye yuko hatarini kufungwa huku wakitoa maelezo tata.

Babu Tale ambaye pia ni mbunge wa Morogoro Kusini ‘anachungulia jela’ kutokana na shauri la maombi lililofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Sheikh Hashim Mbonde dhidi yake na kampuni yao inayojihusisha na masuala ya burudani.

Sheikh Mbonde amefungua shauri hilo akiiomba mahakama iamuru Babu Tale afungwe jela kama mfungwa wa madai katika kutekeleza hukumu yake ya kumlipa fidia kwa kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake, baada ya kushindwa kumlipa fidia ya zaidi ya Sh210 milioni zilizobaki kati ya Sh250 milioni walizoamuriwa na Mahakama kumlipa.

Hata hivyo, Babu Tale ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Tip Top Connections Company Limited amefungua shauri la maombi ya kibali cha kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu hiyo nje ya muda.

Sheikh Mbonde anayewakikishwa na Wakili Michael Mwambeta amemwekea Babu Tale pingamizi dhidi ya maombi hayo, ambayo yamesikilizwa kwa njia ya maandishi’.

Shauri hilo la maombi ya madai namba 467 ya mwaka 2022 la Sheikh Mbonde la amri ya kufungwa Babu Tale linalosikilizwa na Jaji Obadia Bwegoge lilitajwa Oktoba 29, lakini Babu Tale na mawakili wake hawakuwepo. Shauri la Babu Tale, maombi ya madai namba 389 ya mwaka 2022, la kuruhusiwa kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa nje ya muda kupinga hukumu hiyo, linalosikilizwa na Jaji Amir Mruma lilitajwa Desemba 6, lakini pia Babu Tale wala mawakili wake hawakuwepo.

Jana, Mwananchi lilimpata mmoja wa mawakili wa Babu Tale, Issa Chundo na kumuuliza sababu za kutokutokea mahakamani mara zote hizo kwa mashauri yote mawili, lakini alisema walikuwepo katika mashauri yote na kuhoji nani alilieleza Mwananchi kuwa hawakuwepo.

“Tuliofanya appearance (tulikuwepo) na tunajua kuhusiana na hizo kesi,” alisema Wakili Chundo na alipoulizwa nani alikuwepo, alijibu kulikuwa na wakili mwingine mwakilishi kutoka ofisini kwao. Hata hivyo, alipoulizwa huyo wakili mwingine alikuwepo wakati gani kama ni kabla ya kesi kuitwa au baada ya kuahirishwa, alibadili maelezo akidai wanafuatilia kesi hizo kwa namna nyingine.

Mashauri hayo kila yalipoitwa mahakamani ulikuwepo upande mmoja wa Sheikh Mbonde. Mashauri yote yamepangwa kuendelea mwakani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live