Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavokali awaburuza Harmonize, Zuchu na Kiba

Mavokaliiii Mavokali awaporomosha Harmonize, Zuchu na Kiba

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mchanga kutoka Bongo Fleva, Mavokali amemshusha supastaa wa muziki Tanzania, Harmonize katika orodha ya wasanii waliosikilizwa zaidi kupitia mtandao wa Spotify katika kipindi cha mwezi Februari.

Mkali huyo wa ngoma ya 'Mapopo' amepanda mpaka nafasi ya tatu akimshusha Konde Boy mpaka nafasi ya nne kwenye orodha hiyo. Zuchu yupo nafasi ya saba huku Alikiba akishika nafasi ya 10.

Wasanii Wa Tanzania wanaosikilizwa zaidi Spotify kwa mwezi Februari 2023;

1. Platnumz - streams 1,353,664

2. Rayvanny - streams 1,003,661

3. Mavokali - streams 663,183

4. Harmonize - streams 635,282

5. Loui - streams 274,168

6. Marioo - streams 246,087

7. Zuchu - streams 196,996

8. Mbosso - streams 129,295

9. Juma Jux - streams 117,908

10. Alikiba - streams 105,783.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live