Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavazi yampoza Martha Mwaipaja

Erg Mwaipaja Martha Mwaipaja.

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya mashabiki wa Mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili Tanzania, Martha Mwaipaja wameonekana kuchukizwa na mwenendo wa Mwimbaji huyo wakidai kwamba amekuwa akivaa mavazi ambayo yapo nje ya kazi yake kama mtumishi wa Mungu anayeaminika.

Wengi wamesema aina ya uvaaji wake wa kuacha kifua wazi, kuvaa nguo fupi kupitiliza na suruali siyo aina ya mavazi anayopaswa kuvaa akiwa kama kioo cha jamii kupitia Injili.

Haya ni baadhi ya maoni ya wadau kwenye posti zake kuhusu mavazi yake. "Ni Injili ama ni show ya urembo?"

"Madam nakupenda hadi nakupenda tena, lakini sasa hizi suruali zinatutisha, sijui lakini nisihukumu."

"Mimi ni mmoja wa watu wanaofatilia nyimbo zako ila unanipa ukakasi kuhusu suala la mavazi yako mtumishi hayana utukufu mbele ya Yesu Kristo."

"Embu irudie asili ya Injili, neno la Mungu linaagiza wanawake mvae vipi, na sisi wanaume tuvae vipi, wewe ni muhubiri kupitia nyimbo zako, sifa mojawapo ya muhubiri lazima awe msomaji mzuri wa neno la Mungu."

"Kwisha habari yako."

"Kiufupi mimi unanikela hapo kwenye mavazi tu kiufupi upo kibiashara zaidi na siyo kumwimbia Bwana."

"Kweli pata pesa tujue tabia yako, pesa ni shetani nimeamini, Martha wa tusikate tamaa leo hii unatuvalia hivi!! huku ni kuitia aibu Injili, watu wengi wanakupenda lakini unatupoteza, hatujivunii wewe tena."

"Acha kuvaa miwani ya ajabu dada yangu, mrudie Mungu wako, pesa si kitu, utajibu nini mbele ya muumba wako!! unatutisha."

Una mtazamo gani juu ya hili?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live