Kufuatia kukamatwa kwa mwanamuziki Sean “Diddy” Combs wiki iliyopita imeripotiwa kuwa mauzo ya nyimbo zake yamepanda na kupata ongezeko kubwa la wasikilizaji katika kazi zake kupitia mitandao ya kuuzia muziki.
Kwa mujibu wa tovuti ya ABC News, imeeleza kuwa kampuni ya Luminate, inayoshughulika na takwimu katika tasnia ya muziki imeripoti kuwa muziki wa Diddy ulipata ongezeko la wasikilizaji asilimia 18.3 kwa wiki iliyoisha.
Sio jambo la kushangaza kuona idadi ya usikilizaji wa muziki ikiongezeka baada ya msanii kukutana na tuhuma flani, utakumbuka mwanamuziki R.Kelly baada ya kutuhumiwa kwa unyanyasaji wa kingono kwa wanawake na wasichana wadogo idadi ya usikilizaji wa ngoma zake iliongezeka mara mbili zaidi.