Mtayarishaji mkongwe na CEO wa zamani wa Death Row Records, Suge Knight ametoa kauli kuwa hatapanda kizimbani kutoa ushuhuda wa nani aliyemuua Tupac Shakur.
Suge Knight alikuwa pembeni ya Tupac kwenye gari siku ambayo anashambuliwa kwa risasi Jijini Las Vegas, Septemba 7 mwaka 1996.
Kwenye sauti ambayo imetolewa na Tovuti ya TMZ ambao walifanya naye mahojiano, Suge Knight amefunguka kwamba hatatoa ushuhuda dhidi ya Keffe D ambaye amekamatwa wiki iliyopita akihusishwa na mauaji hayo. Aidha Suge Knight ambaye alikuwa swahiba wa Tupac, amesema muuaji wa Tupac Shakur siye ambaye polisi wanamdhani.
Kauli hizi za Suge Knight zimeibua maswali mengi kwenye vichwa vya wafuatialiji wa Kesi hii, wengi wakihoji kwamba inawezekanaje akashindwa kutoa ushuhuda kwenye jambo ambalo limechukua uhai wa rafiki yake?